Kusudi kuu la mchezo huu ni kuboresha ubunifu na kumbukumbu kutumia matofali ya ujenzi ya mbao kwa njia ya kucheza kwa watoto.
Katika huu mchezo, unapaswa (mchezaji) kujenga vitu ambavyo vinajulikana kutoka na maisha ya kila siku. (Kwa mfano majengo, wanyama, na kadhalika). Vitalu vinavyohitajika kwa ujenzi vinafaa kusafirishwa kwa kutumia magari anuwai (magari, treni, ndege). Matofali ya mbao yafaayo, yanapaswa kuchukuliwa kutoka kwa magari yanayoyasafirisha na kuwekwa karibu na eneo lao la lengo.
Mchakato wa kutatua kiwango fulani unaweza kugawanywa kwa sehemu mbili zifuatazo:
- Sehemu ya kwanza unapaswa kukariri takwimu ya rangi ya maeneo lengwa ya matofali ya ujenzi. Unaweza tumia muda unaotaka katika sehemu hii.
- Baada ya hayo, kwenye sehemu ya pili takwimu zinapotea punde tu tofali la kwanza linanyakuliwa kutoka kwa gari. Kisha matofali yafaayo yanapaswa kuchaguliwa na kushukishwa kwenye maeneo lengo yaliyochanguliwa hapo awali kulingana na kipengee (rangi, sura) kinachomechi nayo.
Ikiwa umekwama, unaweza pata usaidizi kwa kubonyeza kitufe chenye alama ya swali. Kwa ktumia usaidizi mara tatu tu, kiwango kizima chaweza kutatuliwa. Kumbuka kuwa matofali yailiyochanguliwa vibaya na pia matumizi ya kitufe cha usaidizi yanapunguza ile kasi ya magari na kuathiri alama ya mwisho. Iwapo ile kasi ya magari itapungua chini ya asilimia sabini na tano, inaweza pandishwa hadi asilimia mia kwa mia kwa kushinikiza ile bar ya kiashiria kasi. Lengo kuu ni kuwa na alama bora zaidi ya mwisho kwenye kila kiwango.
Kuna mfano unaoapatikana kwenye kiwango cha kwanza ambao unaweza kukusaidia kuelewa misingi ya mchezo huu.
Vipengele vya mchezo huu:
- Hatua mia moja na moja tofauti na zenye ungumu wa viwango vitatu
- Matofali ya ujenzi kumi na tano yaliyo na maumbo tofauti na yenye rangi tano katika kila kiwango
Ilisasishwa tarehe
25 Jul 2024