Rekodi matukio yote ukitumia Kamera ya Pixel iliyobuniwa upya kikamilifu na upige picha pamoja na kurekodi video maridadi ukitumia vipengele kama vile Fifiza, Shabaha ya usiku, Mpito wa Muda na Kutia Ukungu Mtindo wa Sinema.
Piga picha za kuvutia
• HDR+ iliyo na Vidhibiti vya Kusawazisha Weupe na Mwanga - Piga picha za kupendeza ukitumia HDR+, hususani katika mandhari yenye mwangaza hafifu au mandhari yaliyomulikwa kutoka nyuma.
• Shabaha ya Usiku - Kamwe hutahitaji kutumia mweko wa kamera yako tena. Shabaha ya usiku huonyesha rangi na vipengee vyote visivyoonekana kwenye giza. Unaweza hata kupiga picha za Kundi la Kilimia ukitumia kipengele cha Upigaji picha za anga!
• Kuza na upige picha safi - Sogeza karibu vitu vilivyo mbali. Kipengele cha Kuza na upige picha safi huboresha picha zako unapovuta karibu.
• Kitia Ukungu Kwenye Maudhui - Weka ukungu bunifu ili vipengee vinavyosogea katika tukio
• Kunasa Vitendo - Weka ukungu bunifu kwenye mandharinyuma huku ukiweka kipengee chako kwenye fokasi
• Ulengaji wa Karibu - Rangi dhahiri na za kupendeza hata kwenye vipengee vidogo zaidi
Video zinazovutia kila unaporekodi
• Rekodi video nzuri zenye ubora wa juu na sauti safi, hata katika sehemu zenye watu wengi, zilizo na mwanga hafifu
• Kutia ukungu mtindo wa sinema - Weka mtindo wa kisinema kwa kutia ukungu mandharinyuma ya kipengee chako
• Kunasa Sinema - Punguza kasi ya mtikisiko wa kugeuza simu yako.
• Picha Pana - Rekodi video za kawaida na za haraka kwa kubonyeza tu kitufe cha kilango cha kamera kwa muda mrefu katika hali chaguomsingi ya kupiga picha.
Vipengele vya Kipekee vya Pixel 8 Pro
• Ubora wa juu wa 50MP - Piga picha zenye ubora wa juu zinazovutia zaidi
• Udhibiti wa Magwiji - Pata udhibiti zaidi wa ubunifu kupitia uwezo wa kurekebisha vitu kama vile fokasi, kasi ya kufunga kilango cha kamera na zaidi
Masharti - Toleo jipya la Kamera ya Pixel linafanya kazi tu kwenye vifaa vya Pixel vinavyotumia Android 14 na matoleo mapya zaidi. Toleo jipya zaidi la Kamera ya Pixel kwenye Wear OS linafanya kazi tu katika vifaa vinavyotumia toleo la Wear OS 3 (na matoleo mapya zaidi) vilivyounganishwa na simu za Pixel. Baadhi ya vipengele havipatikani kwenye vifaa vyote.
Ilisasishwa tarehe
22 Nov 2024