Family Link kutoka Google ni programu ya vidhibiti vya wazazi ambayo inakuwezesha kuimarisha usalama wa familia yako mtandaoni. Zana za Family Link ambazo ni rahisi kutumia hukuwezesha kuelewa jinsi mtoto wako anavyotumia muda kwenye kifaa chake, kuona mahali kifaa chake kilipo, kudhibiti mipangilio ya faragha na mengineyo.
Ukitumia Family Link, unaweza:
Kuweka Sheria Dijitali za Msingi
• Kuweka vikomo vya muda wa kutumia kifaa — Family Link hukuwezesha kuweka wakati wa kupumzika kwenye kifaa cha mtoto wako na vikomo vya muda wa kutumia programu, ili umsaidie kuweka uwiano mzuri.
• Kumwelekeza mtoto wako kwenye maudhui yanayoambatana na umri wake — Kuidhinisha au kuzuia programu ambazo anataka kupakua. Family Link pia hukuwezesha kuchagua hali ya kutumia YouTube inayomfaa mtoto wako: matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube au YouTube Kids.
Kudhibiti na kuimarisha usalama wa akaunti ya mtoto wako
• Kulinda faragha yake — Kipengele cha kudhibiti ruhusa katika Family Link hukuwezesha kufanya uamuzi bora kuhusu data ya mtoto wako. Angalia na udhibiti ruhusa za tovuti na viendelezi vinavyofikiwa kupitia Chrome pamoja na za programu zinazopakuliwa kwenye kifaa cha mtoto wako.
• Linda akaunti yake — Family Link hukuwezesha kudhibiti mipangilio ya akaunti na data ya mtoto wako. Kama mzazi, unaweza kusaidia kubadilisha au kuweka upya nenosiri la mtoto wako akilisahau, kubadilisha taarifa zake binafsi au hata kufuta akaunti yake panapohitajika.
Kuunganishwa popote ulipo
• Kuona mahali mtoto wako alipo — Ni muhimu kuweza kuwapata wanafamilia yako popote walipo. Ukitumia Family Link, unaweza kuona mahali watoto wako walipo kwenye ramani moja, mradi wamebeba vifaa vyao.
• Kupata arifa — Family Link hukutumia arifa muhimu ikiwa ni pamoja na wakati mtoto wako anawasili au kuondoka mahali fulani. Unaweza pia kupigia vifaa na kuangalia muda wa matumizi ya betri uliosalia kwenye kifaa.
Maelezo Muhimu
• Zana za Family Link hutofautiana kulingana na kifaa cha mtoto wako. Angalia orodha ya vifaa vinavyooana katika https://families.google/familylink/device-compatibility/
• Ijapokuwa programu ya Family Link hukusaidia kudhibiti vipakuliwa na ununuzi wa mtoto wako kutoka Google Play, hatahitaji idhini yako kusakinisha masasisho ya programu (yakiwemo masasisho yaliyo na ruhusa nyingi zaidi), programu ulizoidhinisha hapo awali au programu zilizoshirikiwa katika Maktaba ya Familia. Isitoshe, idhini za ununuzi zitatumika tu mtoto wako anaponunua kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play na hazitatumika anapofanya ununuzi kupitia mifumo mbadala ya utozaji. Wazazi wanapaswa kukagua mara kwa mara programu zilizosakinishwa na ruhusa za programu za watoto wao katika Family Link.
• Unapaswa kukagua kwa makini programu zilizo kwenye kifaa cha mtoto wako kinachodhibitiwa na uzime zile usizotaka atumie. Kumbuka, huenda usiweze kuzima baadhi ya programu zilizosakinishwa awali k.v. Google Play, Google, n.k.
• Ili uone mahali kifaa cha kijana au mtoto wako kilipo, ni lazima kiwe kimewashwa, kimetumika hivi majuzi na kimeunganishwa kwenye intaneti kupitia data au wifi.
• Vidhibiti vya wazazi vya Family Link vinapatikana tu kwenye akaunti za Google zinazodhibitiwa. Kwenye Akaunti za Google zinazodhibitiwa, watoto hupata uwezo wa kufikia bidhaa za Google k.v. Tafuta, Chrome na Gmail na wazazi wanaweza kuweka sheria dijitali za msingi ili kuwasimamia.
• Ijapokuwa Family Link hukupa zana za kudhibiti hali ya mtoto wako mtandaoni na kuimarisha usalama wake, haifanyi intaneti kuwa salama. Family Link haiwezi kuamua maudhui yanayopatikana kwenye intaneti, lakini inaweza kuwapa wazazi fursa ya kuamua kuhusu jinsi watoto wao wanavyotumia muda kwenye vifaa vyao na kubaini njia ya kudumisha usalama wa mtandaoni inayofaa familia zao.
Ilisasishwa tarehe
21 Nov 2024