Tekeleza shughuli nyingi zaidi ukitumia programu ya simu ya Google Majukumu. Dhibiti, nakili na ubadilishe majukumu ukiwa popote pale, wakati wowote, ukitumia mambo ya kushughulikia ambayo yanasawazishwa katika vifaa vyako vyote. Kuunganishwa kwake na Gmail na Kalenda ya Google kunakusaidia kutekeleza majukumu yako—haraka.
Nakili majukumu haraka ukiwa popote
• Unda orodha ya majukumu yako kwa kupanga mambo ya kushughulikia yaliyo muhimu zaidi
• Angalia, badilisha na udhibiti majukumu popote ulipo ukitumia kifaa chochote
• Dhibiti majukumu yaliyoundwa kwenye Gmail au Kalenda kwenye wavuti ukitumia kifaa chako cha mkononi
Ongeza maelezo na uunde majukumu madogo
• Gawa majukumu yako yawe majukumu madogo
• Ongeza maelezo kuhusu kazi unayofaa kuangazia zaidi
• Badilisha maelezo kuhusu majukumu yoyote kadri kazi yako inavyoendelea
Angalia majukumu yaliyoongezwa kwenye barua pepe
• Ongeza jukumu moja kwa moja kwenye Barua pepe ya Gmail
• Angalia majukumu yako kwenye kidirisha cha pembeni cha Gmail
• Fuatilia jukumu hadi kwenye barua pepe chanzo
Endelea kufuatilia shughuli zako kwa kuweka tarehe za kukamilisha na arifa
• Wekea kila jukumu lako tarehe ya kukamilisha ili ikusaidie kutimiza malengo yako
• Panga majukumu yako kwa tarehe ya kukamilisha au weka kipaumbele kwa kuburuta na kudondosha
• Pokea arifa za vikumbusho kuhusu tarehe za kukamilisha ili uendelee kufuatilia majukumu yako
Ni Sehemu ya G Suite
• Tumia mkusanyiko bora wa programu mahiri na thabiti za Google katika biashara yako
• Tumia kipengele cha AI kutoka Google ili kuleta maarifa na uchanganuzi wa data kwa kila mfanyakazi
• Ungana na timu yako kwa urahisi ukitumia mkusanyiko mmoja: Gmail, Majukumu, Kalenda na huduma zingine
Anza kudhibiti usimamizi wa majukumu yako kwa kusakinisha programu ya simu ya Google Majukumu. Anza kudhibiti orodha yako ya mambo ya kushughulikia popote ulipo kwa kutumia programu ya kupanga Majukumu kutoka Google.
Ilisasishwa tarehe
21 Nov 2024