Zana za Ufikivu za Android ni mkusanyiko wa programu za ufikivu zinazokusaidia utumie kifaa chako cha Android bila kukitazama au kwa kutumia kifaa cha swichi.
Zana za Ufikivu za Android zinajumuisha:
• Menyu ya Ufikivu: Tumia menyu hii kubwa iliyo kwenye skrini ili kufunga simu yako, kudhibiti kiwango cha sauti na mwangaza, kupiga picha za skrini na zaidi.
• Chagua ili Izungumze: Chagua vipengee kwenye skrini yako na usikie vikisomwa kwa sauti.
• Kisoma skrini cha TalkBack: Pata maelezo yanayotamkwa, dhibiti kifaa chako ukitumia ishara na uandike ukitumia kibodi ya skrini ya nukta nundu iliyo kwenye skrini.
Ili uanze kutumia:
1. Fungua programu ya Mipangilio ya kifaa chako.
2. Chagua Ufikivu.
3. Chagua Menyu ya Ufikivu, Chagua ili Izungumze au TalkBack.
Zana za Ufikivu za Android zinahitaji toleo la Android 6 (Android M) au toleo jipya zaidi. Ili utumie kipengele cha TalkBack kwenye Wear, utahitaji toleo la Wear OS 3.0 au toleo jipya zaidi.
Taarifa ya Ruhusa
• Simu: Zana za Ufikivu za Android huchunguza hali ya simu ili ifanye matangazo yaoane na hali yako ya kupiga simu.
• Huduma ya Ufikivu: Kwa sababu programu hii ni huduma ya ufikivu, inaweza kuchunguza vitendo unavyotekeleza, kuleta maudhui ya dirisha na kuona maandishi unayoandika.
• Arifa: Ukiwasha ruhusa hii, kipengele cha TalkBack kinaweza kukuarifu kuhusu masasisho.
Ilisasishwa tarehe
18 Nov 2024