Opera ni kivinjari cha haraka na salama cha Android yako, iliyo na milisho ya habari iliyowashwa, kizuizi cha matangazo na VPN ya bure.
★ Vipengele bora ★
● Zuia matangazo kwa ajili ya kuvinjari haraka zaidi:
Kizuiaji matangazo asili cha Opera hukusaidia vizuri kuondoa matangazo yanayokatiza matumizi na kupakia kurasa zako haraka zaidi ili kuratibu hali yako ya kuvinjari.
● VPN ya bure, isiyo na kikomo ya ndani:
Boresha faragha na usalama kwa VPN ya ndani na bila malipo. Washa Opera VPN katika hali ya faragha na anwani yako ya IP itabadilishwa kwa ile ya kweli ili kukusaidia kuepuka eneo usilokusudia na ushiriki wa taarifa ya utambulisho.
● QR ya ndani na skana ya msimboupau :
Fikia skana ya QR ya ndani na msimboupau. Gonga tu upau wa kutafuta na skana ipo upande wa kulia. Elekeza kamera kwenye msimbo/msimboupau wa QR na itachanganuliwa kiotomatiki.
● Flow: huunganisha vifaa vyote bila tatizo :
Kipengele maarufu cha Flow kinaruhusu faili, viungo au picha unazoshiriki haraka zionekane kwenye vifaa vyako vyote ulivyowezesha Flow na kukuruhusu kutumia iPhone, simu ya Android, tableti na kompyuta bila tatizo.
● Mlisho wa habari ulioboreshwa:
Inaendeshwa na mtambo mahiri zaidi wa habari za AI, mlisho wa habari uliowashwa tena hukuruhusu kutelezesha kwenye uteuzi wa idhaa za habari zilizoboreshwa ndani ya kivinjari, jisajili kwenye mada zinazokuvutia na uhifadhi hadithi ili usome baadaye. Fuatilia habari za AI zilizoratibiwa haswa zilizoboreshwa kwa ajili yako.
● Hali ya usiku:
Hali ya usiku ya Opera hukupa chaguo za mwangaza zinazoweza kurekebishwa ili kupata hali bora zaidi ya kusoma katika giza na usumbufu mdogo zaidi wa macho. Hali ya usiku inafikiwa kwa urahisi kutoka kwenye menyu kuu.
● Dhibiti manenosiri na kadi za mikopo za kujaza kiotomatiki:
Chagua kuingia kwa ajili ya kuhifadhi kiotomatiki manenosiri tovuti kwa tovuti na kujaza kwa usalama taarifa yako ya malipo kwa ajili ya ununuzi wa mtandaoni.
● Kuvinjari kwa faragha:
Tumia vichupo vya faragha kuvinjari kwa njia fiche popote kwenye Intaneti bila kuacha historia kwenye kifaa chako. Badilisha kwaurahisi ili kutumia kuvinjari kwa faragha na kwa kawaida katika matunzio ya kichupo.
● Soma kwenye skrini yoyote bila tatizo:
Kivinjari cha Opera kinajumuisha mpangilio wa ukubwa wa maandishi unaokusaidiakutumia kurasa kulingana na mapendeleo yako ya kusoma. Muhimu zaidi, inafanya kazi vizuri na kipangele chetu cha kupanga maandishi kiotomatiki kwa hali yako ya kipekee ya kusoma.
● Dhibiti vipakuliwa kwa urahisi:
Kidhibiti chetu kipya cha upakuaji hurahisisha na kuharakisha kupakua faili kuliko awali! Unaweza kupanga na kushiriki kila kipengee kilichopakuliwa, kuvifuta kwenye simu au kuviondoa kwenye orodha ya vipakuliwa kwa kutelezesha haraka upande wa kulia au kushoto. Hata tunatumia upakuaji wa chinichini wakati ambapo una upakuaji unaoendelea lakini unahitaji kufungua programu nyingine!
● Sawazisha vifaa vyako vya Opera:
Jipe idhini ya kufikia kwenye maalamisho yako yote, njia za mkato za Upigaji Haraka na vichupo vilivyo wazi kutoka kwenye vifaa vyako vingine vinavyotumia Opera. Opera kwenye Android sasa inaweza kusawazisha kwa urahisi kwa kivinjari cha Opera ya kompyuta.
Fanya zaidi na Opera: https://www.opera.com/mobile/android
Opera Mini inaweza kuonyesha matangazo kutoka Facebook. Ili kupata maelezo zaidi, tazama https://m.facebook.com/ads/ad_choices
Wasiliana:
Twitter – http://twitter.com/opera/
Facebook – http://www.facebook.com/opera/
Instagram – http://www.instagram.com/opera
Sheria na Masharti
Kwa kupakua programu hii, unakubali Makubaliano ya Leseni ya Mtumiaji kwenye http://www.opera.com/eula/mobile. Pia, unaweza kujifunza jinsi Opera inavyotumia na kulinda data yako katika Taarifa yetu ya Faragha kwenye https://www.opera.com/privacy.
Ilisasishwa tarehe
24 Nov 2024